Friday, April 6, 2018

 
TAMBUA/ELEWA UMUHIMU WA MALAIKA WA VITA WANAVYOWEZA KUTUSAIDIA KUPIGANA VITA VYA KIROHO.


Lengo kuu la kujifunza somo hili ni kumwezesha mwombaji kupata maarifa yatakayomsaidia kujibiwa maombi yake kwa wakati.
1.VITA VYA KIROHO.
Ni vita inayofanyika katika ulimwengu wa roho.Ulimwengu wa roho ni mahali ambapo roho zinaishi ( habitat of spirits), huu ulimwengu wa roho umegawanyika sehemu kubwa mbili:-

1.Ulimwengu wa roho katika nuru
2.Ulimwengu wa roho katika giza

1.Ulimwengu wa roho katika nuru
Ni ulimwengu ambao Mungu Mtakatifu na malaika( ikijumuisha wenye uhai 4 na wazee 24) wanaishi.Mtu yoyote aliyeokoka anauwezo wa kuishi hili eneo kwa msaada wa Roho Mtakatifu, ili uweze kulifahamu vizuri hili eneo unamuhitaji Roho Mtakatifu maana yeye ndiye mwenyeji wa hili eneo.

      "Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu" (WAEFESO 2:6)
Kwahiyo kumbe yoyote aliyeokoka anaweza akaishi katika ulimwengu wa roho katika nuru hata akiwa bado yuko duniani anaishi!


2.Ulimwengu wa roho katika giza
Ni eneo ambalo Shetani, majini, mapepo, mizimu na kila aina za roho chafu zinaishi.Mtu yoyote aliyeokoka amepewa mamlaka ya kulitawala hili eneo kuanzia Shetani na majeshi yake yote.

    "Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru" (LUKA 10:19)
Kumbe kwasababu tumeketishwa na Kristo katika ulimwengu wa roho tumewekwa juu ya ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo ( WAEFESO 1:20-23).

Njia ya maombi pekee ndiyo ambayo inaweza kumsaidia mwamini aliyeokoka kupigana vita vya kiroho.Maombi yoyote kwa asili ni vita haijalishi hayo maombi unayoomba mbele za Mungu unaomba kwa kupekeka hoja mbele za Mungu au kwa njia ya mahojiano, unaweza ukafanya maombi kwa njia ya mahojiano na Mungu kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Lakini wakati wa kupokea majibu ya maombi uliyoyaomba ni vita! Jiulize haya  maswali wewe mwenyewe kwani ni maombi mangapi uliomba kwa Mungu akakuhaidi kabisa atakupa lakini mpaka sasa hauoni majibu ya maombi uliyoomba? Unafikiri ni kwanini? Si unaona sasa ulizungumza na Mungu kwa njia ya mazungumzo njia ya amani kabisa lakini angalia sasa kwenye eneo la kupokea majibu yako.Utagundua sasa kumbe kati ya mapmbi kumi uliyoomba umejibiwa moja. Katika siri ambayo watoto wa Mungu wengi hawaifahamu katika maombi ni hii kutojua kwamba Shetani anapigana sana vita na eneo la kupokea majibu ya maombi wanayoomba!

Kuna hatua 2 za maombi ambazo huwa zinapitia mpaka kufikia hatua ya kujibiwa maombi uliyoomba:-

1.Wakati unaomba maombi yako kwenda mbele za Mungu.
2.Wakati unasubiri majibu ya maombi uliyoomba kutoka kwa Mungu.

-Waombaji wengi wamefaulu hatua ya kwanza ya kupeleka hoja zao mbele za Mungu. Japokuwa maombi haya bado ni vita pamoja na kwamba unampelekea Mungu maombi au hoja zako. Utanielewa nina maana gani.Lakini waombaji wengi wamefeli kwa kiasi kikubwa katika hatua ya pili ya kupokea majibu ya maombi waliyoomba mbele za Mungu. Wengi wakimwomba Mungu maombi yao Mungu akasema atawapa wanaridhika, wanaacha kuomba wanarelax (wanajiachia ) wakifikiri Mungu ndiye atawashughulikia upatikanaji wa maombi wanayoyaomba mpaka yaonekane katika macho ya damu na nyama. Hee hee kumbuka kanuni ya kiroho jinsi ilivyo pamoja na kwamba Mungu atakupa ruhusa ya kukupa ulichohitaji ila mwenye kazi ya kuumba ulichokihitaji ni wewe ili kiweze kutokea kwa macho ya damu na nyama.

Hii imesababisha waombaji wengi kukata tamaa kwasababu wanafikiri Mungu ni mwongo! Wengine wanafikiri ni majaribu Mungu anawapitisha lakini kumbe sivyoo. Mungu hapendi watu wake waishi kwa shida wala majuto Mungu anawapenda watu wake anataka waishi kwas furaha na amani. Na Mungu huwa anaachilia jaribu kwa kusudi maalumu. Kwahiyo utakubaliana na mimi kwamba jaribu ni " special case" kwasababu maandiko yanasema Mungu anatuwazia mema kila iitwapo leo maana yake hata kabla hujaomba kusudi la Mungu ni kukuona unafanikiwa kwenye maisha yako.

Natamani upate hasira ndani yako kuanzia sasa kwamba mwenye shida ya kutojibiwa maombi yako ni wewe mwenyewe. Wewe ukisimama sawa sawa nilazima ulichoomba mbele za Mungu ukipate madamu tuu yeye Mungu ameruhusu upate ulichoomba. Shetani anafahamu kabisa Mungu huwa anaachilia majibu kwenye ulimwengu wa roho ili watoto wake wakipate. Shetani kazi yake huwa anahakikisha anapigana kwenye ulimwengu wa roho ili usipate ulichoomba kwasababu amejaa hila! Maandiko yanasema ivi:-
      "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka" (MATHAYO 11:12)

Unaona sasa! Unaelewa nini maana ya ufalme wa mbinguni?
Tusome MATHAYO 5:9- 10 angalia inavyosema:-
       "Basi ninyi salini hivi, Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni"

Umeona sasa ufalme wa mbinguni kuja haimaanishi Mungu ashuke pamoja na malaika zake hapa duniani hapana! Mungu anautaratibu katika utawala Mungu ni Roho (YOHANA 4:24) hawezi kuja duniani kutawala bila kutumia mwili( mtu/mwanadamu) ni lazima amtumie mwanadamu ili aweze kutawala hiyo ni kanuni aliyojiwekea. Mungu anakanuni zake kanuni aliyoiweka yeye mwenyewe huwa haitengui hata siku moja hiyo ni kanuni aliyoiweka mwenyewe nilazima aifuate. Unaweza kujiuliza maswali kwanini Mungu hakuamua kumtuma Yesu aje kama nguvu fulani ivi haionekani kwa macho ikawa ni sauti tuu iseme mimi ni mwana wa Mungu nimeagizwa kuwaokoa wanadamu. Lakini unafikiri Mungu angeamua kufanya hivyo angeshindwa? Kwahiyo Mungu anaweza kufanya chochote lakini anaheshimu sana kanuni na taratibu alizojiwekea yeye mwenyewe.

Kwahiyo sasa kumbe Mungu anamtumia mtu kuushusha ufalme wake hapa duniani. Lakini kuuteka huo ufalme uje duniani mwenye nguvu peke yake ndiye anayeweza kuuteka! Sasa ufalme wa Mungu umebeba mambo mengi sana ndani yake lakini elewa tuu ufalme wa Mungu umebeba kila kitu chenye kumfanikisha mwanadamu! Maombi ya aina yoyote unatoyaomba yamebebwa ndani ya ufalme wa Mungu! anayetakiwa kuushusha huo ufalme ni wewe.



2.MALAIKA
Ni viumbe ambao wanamfano wa mwili wa wanadamu (Mwanzo 32:24-30, Ebrania 13:2), wanaweza kugusika ni viumbe ambao wanaushirika wa karibu sana na Mungu. Malaika wa vita kazi yao kubwa ni kumsaidia mwanadamu kupigana vita vya kiroho.Kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanaleta majibu ya maombi uliyoomba kutoka kwa Mungu.
   
        "Malaika wa BWANA hufanya kituo, Akiwazunguka wamchao na kuwaokoa" (ZABURI 34:7) 
Kwahiyo katika ulimwengu wa roho, wako malaika ambao wanamsaidia mwanadamu kupigana vita vya kiroho wale wamchao! Watu wengi sana wanaamini uwepo wa Roho Mtakatifu hawaamini uwepo wa malaika wanaowasaidia kupigana vita vya kiroho.Kumbuka Roho Mtakatifu anatusaidia kuomba maombi tuliyonayo (Rum 8:26) lakini kwenye eneo la kuyaumba majibu ya maombi uliyopokea kutoka kwa Mungu muhusika ni wewe. Ndio maana maandiko yanasema ninyi ni miungu. Yaani kwa mfano unapoingia kumwomba Mungu akupe gari, unahitaji msaada wa Roho Mtakatifu ili akusaidie kuomba mbele za Mungu. Roho Mtakatifu anakuja na majibu kutoka kwa Mungu kwamba Mungu atakupa either siku fulani au mwezi fulani au mwaka  fulani. Hapo umepokea majibu ya maombi lakini mwenye kazi ya kusimamia hilo gari uliloomba mpaka litokee katika macho ya damu na nyama ni wewe mwenyewe.


   DANIELI 10:11-15 inasema ivi:-
           "Akamwambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima, maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka. Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli, kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekesha mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa, nami nimekuja kwaajili ya maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja, bali tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia, nami nikamwacha huko paoja na wafalme wa Uajemi".

Sasa umeona kumbe Danieli alijibiwa maombi yake tangu siku ya kwanza lakini majibu ya maombi yaliyokuwa yamebebwa na malaika yalipingwa na ufalme wa Uajemi siku ishirini na moja kwasababu malaika alikuwa hana nguvu ya kupigana na huo ufalme. Kilicho msaidia huyo malaika ni malaika Mikaeli ndio akapata upenyo wa kutoroka kumpelekea Danieli majibu ya maombi aliyoyaomba. Lakini kumbuka Danieli alikaa siku ishirini na moja kwenye maombi. Swali la kujiuliza mwenye makosa ni nani? Je ni Mungu ambaye alitoa majibu kwa wakati tangu siku ya kwanza ya maombi ya Danieli? Je ni malaika ambaye alikuwa ni mdhaifu kupigana vita juu ya ufalme wa Uajemi? Au ni Danieli ambaye hakuwa na ufahamu wa kutambua katika ulimwengu wa roho kuna hila za Shetani?

Majibu tunayapata moja kwa moja kuwa Danieli kilichosababisha acheleweshewe majibu ya maombi yake ni kwamba hakuwa na ufahamu juu ya maombi ya vita. Kwasababu alikuwa na mamlaka kabisa ya kuamuru ufalme wa Uajemi upigwe ili maombi yake yajibiwe kwa wakati.Kwahiyo kumbe Danieli angefanya maombi ya vita angepokea majibu ya maombi yake siku ile ya kwanza alipoingia kuomba.


Mambo muhimu ya kufahamu juu ya malaika wa vita
1.Malaika wa vita wanabeba wasifu wa mwombaji.
2.Wanasikiliza amri ya mwombaji.
3.Utendaji kazi wao unategemeana sana na mazingira ya kiroho ya mwombaji.

Wasifu wa malaika wa vita anavyotakiwa kuwa katika ulimwengu wa roho
1.Anatakiwa awe na vazi la kisasi
2.Anatakiwa awe amejifunga kweli kiunoni
3.Anatakiwa awe amejifunfa deraya/dirii kifuani
4.Anatakiwa avae utayari miguuni
5.Anatakiwa awe ameshika ngao mkono wake wa kushoto
6.Anatakiwa awe na upanga wa roho ameushika mkono wake wa kulia
7.Anatakiwa awe na chepeo ameivaa kichwani



WAEFESO 6:10- 17 inasema ivi:-
         "Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi wa pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwasababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa injili ya amani, zaidi ya yote mkitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chepeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu."

Paulo alijua kwenye ulimwengu wa roho kuna hila za Shetani na iko vita ndio maana aliwaambia Waefeso twaeni silaha zote za Mungu! Kwasababu alijua wako malaika ambao wanatakiwa wabebe huo wasifu wa hizo silaha za vita ili waweze kushinda vita kwenye ulimwengu wa roho! Sasa inapoingia kwenye maombi ya vita nilazima uvae silaha zote za vita. Ili malaika wako wanaokusaidia kupigana vita vya kiroho wasipigwe, washinde vita. Kwasababu hao malaika watachukua wasifu wako, silaha ulizovaa ndio watakazo zivaa, kama utaingia kwenye hayo maombi ukawa umeshika upanga tuu peke yake ujue utakuwa na uwezo wa kuua lakini mishale ya moto ya adui ikija utashindwa kuizuia kwasababu hauna ngao.Kwahiyo kuna umuhimu mkubwa wa kuvaa silaha zote za vita ili uweze kupigana vita vizuri vya kiroho na kushinda ili majibu yako yaje kwa wakati!


MBO YA KUZINGATIA UNAPONINGIA KUPIGANA VITA VYA KIROHO
1.Hakikisha unapoingia kwenye maombi ya vita uwe na WIVU ambalo ndio VAZI LA KISASI linalovaliwa mwili mzima.
KISASI
Ni hali ya kuchukia kuonewa na Shetani juu ya jambo ambalo amelifunga kwenye ulimwengu wa roho.Inawezekana ikawa ni kufeli kwenye masomo Shetani amefunga, inawezekana ikawa ni roho mbaya za kurithi Shetani amefunga kwenye ulimwengu wa roho. Ili ushinde vita unatakiwa kuichukia hali mbaya uliyonayo ya kutofanikiwa hiyo itakupa nguvu ya kufanikiwa katika vita unayoiendea.(YAKOBO 4:7)
         
              "Akajivika haki kama deraya kifuani, na chepeo cha wokovu kichwani pake, akajivika mavazi ya kisasi yawe mavazi yake, naye alivikwa wivu kama joho" (ISAYA 59:17).

2.Hakikisha unapoingia kwenye maombi ya vita unakuwa na NIA ya kupigana hiyo vita ambayo ndiyo KWELI inayovaliwa kiunoni.
NIA
Ni kiu ya kutaka kuona kuona kitu kinaenda kufanyika katika ulimwengu wa roho.Kwahiyo muombaji yoyote anapoingia kwenye vita vya kiroho nilazima awe na nia, haitakiwi unapoingia kwenye vita vya kiroho kukata tamaa. Inaweza ikawa unaingia kwenye maombi ya kuvunja madhabahu za miungu kwenye ukoo wako inatakiwa uwe na nia mpaka uone hizo madhabahu zinazokufuatilia za ukoo wako zinavunjika.

        " Kwahiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi, mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wa Yesu Kristo" (1PETRO 1:13)
Kwahiyo unatakiwa kuwa na nia unapoenda kupigana vita nia ndiyo iliyomsaidia Yesu kulitimiza kusudi la Mungu alipokuwa duniani!
     
          "Iweni na nia hiyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo ndani ya Kristo Yesu" (WAFILIPI 2:5).

3.Hakikisha unapoingia kwenye maombi ya vita unakuwa na haki ambayo ni DIRII/DERAYA YA HAKI inayo valiwa kifuani.
HAKI
Ni uhalali wa kupokea kitu ambacho unastahili kukipokea. Mtu mwenye dhambi haruhusiwi kupigana vita vya kiroho! Haki inapatikana kwa njia ya toba, Hakikisha hauingii kwenye maombi ya vita kama haujaomba rehema .
          "Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii" (YAKOBO 5:16b). Haki inapatikana kwa kuomba rehema hakikisha hauingii kwenye maombi ya vita ukiwa haujaomba rehema.

4.Hakikisha unapoingia kwenye maombi ya vita uwe na AMANI ambayo ndio UTAYARI unavaliwa miguuni.(ISAYA 52:7)
            "Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao."(WAEBRANIA 12:14)
Hakikisha unapoingia kwenye maombi ya vita uwe na amani na watu wote usiingie kwenye maombi ya vita huku ukiwa unavinyongo na watu, usiingie kwenye maombi ya vita ukiwa umewabeba watu moyoni, usiingie kwenye maombi ya vita ukiwa na uchungu moyoni waachilie hao watu moyoni mwako na uwasamehe ndipo uingie kwenye maombi ya vita.

5.Hakikisha unaloingia kwenye maombi ya vita uwe na IMANI ambayo ndio ngao inashikwa mkono wa kushoto.
           "zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yenye moto ya yule mwovu" (WAEFESO 6:16)

            "Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu, na huku ndiko kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu."(1YOHANA 5:4)
Hakikisha unaingia kwenye maombi ya vita ukiwa na imani usiingie kwenye maombi ya vita wakati hauamini hiyo vita utashinda.

6.Hakikisha unapoingia kwenye maombi ya vita uwe UMEOKOA ambayo hiyo ni CHEPEO inavaliwa kichwani.(ISAYA 59:17)
           "Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani, na upendo, na chepeo yetu iwe tumaini la wokovu" (1THESALONIKE 5:8)
Kwahiyo usiingie kwenye maombi ya vita ukiwa haujaokoka.Yaani hujamkiri Yesu kuwa ni Bwana na kuamini Mungu alimfufua katika wafu (WARUMI 10:9)
Kwahiyo kama hujaokoka hauruhusiwi kupigana vita vya kiroho aliyeokoka peke yake ndiye mwenye haki ya kupigana vita vya kiroho!

7.Hakikisha unapoingia kwenye maombi ya vita unakuwa na NENO LA MUNGU ambalo ndio UPANGA WA ROHO unashikwa mkono wa kulia.
                  "Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali, katika kivuli cha mkono wake amenisitiri, naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa, katika podo lake amenificha, (ISAYA 49:2)

                  "Kwasababu hiyo nimewakata-kata kwa vinywa vya manabii, nimewaua kwa maneno ya kinywa changu, na hukumu yangu ikatokea kama mwangaza" (HOSEA 6:5)
Kwahiyo unapoingia kupigana viga vya kiroho hakikisha unakuwa na neno la Mungu kwasababu maandiko yanasema neno la Mungu huwagawa nafsi na roho na mafuta. Ni hakika unapotumia NENO la Mungu kwenye maombi ya vita Mungu anafanya! Kwa mfano ni wachawi ndio wametawala kwenye ukoo wako/ mji wako unaweza kuingia kwenye maombi kwa kutumia neno la Mungu linalosema "Usimwache meanamke mchawi aishi" jifunze kutumia neno unapoingia kwenye maombi ya vita. Usiingie kwenye maombi ya vita kama hauna neno la Mungu.



Ili maombi yako yajibiwe kwa wakati nilazima uzingatie haya mambo 7 unapoingia kwenye maombi ya vita.Kwasababu malaika wa vita huwa wanabeba wasifu/ mfano wa mtu anayeingia kupigana hiyo vita kwahiyo kama ikitokea haujavaa viatu ambao ni Utayari malaika naye hatavaa, usipovaa chepeo malaika naye hatavaa, usipokuwa na upanga naye malaika hatashika, kadhalika na silaha nyingine zote.Angalia sasa kama malaika akiwa kwenye ulimwengu wa roho hana silaha zote za vita.Kwanza anakuwa dhaifu, na anapokosa nguvu anashindwa kurejesha majibu ya maombi uliyoomba.

Zaidi sana kinachotokea malakia wa vita akikosa nguvu ya kupigana na falme za giza kwenye ulimwengu wa roho, unaweza ukapata majibu ya maombi yako kwa kuchelewa sana kama ilivyotokea kwa Danieli. Au usipate majibu ya maombi yako kwa kunyang'anywa majibu ya maombi yako ambayo umeomba. Huenda uliyaangaikia kwa kufunga na kufanya maombi ya mda mrefu. Hapo ndipo huwa unafika wakati waokovu wengi wanakata tamaa nakufikiri Mungu amewaacha, na Mungu anasikitika anawahurumia kwasababu wamekosa kuwa na maarifa! (ISAYA 5:13)
Ngoja  nikupe siri hii hakuna kilichochema kinachotoka kwa Ibilisi kila kilichochema kinatoka kwa Mungu!
                 "Kila kutoa kuliko kwema , na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kibadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka" (YAKOBO 1:17) 
Shetani amejaa hila lengo lake kubwa ni kuhakikisha ulichomwomba Mungu hakitokei katika macho ya damu na nyama kwenye maisha yako. Kwahiyo sasa unapoingia kwenye maombi na hauna silaha za vita, malaika wa vita anakuwa dhaifu, kinachotokea ananyang'anywa majibu ya maombi yako na malaika wa kipepo halafu yanahifadhiwa katika ulimwengu wa giza!  Unajua ni kwanini watu wakiendwa kwa waganga wakienyeji kuomba mali, fedha, utajiri, magari, kuwa na akili darasani, kuwa na upako na miujiza wanapata? Kwasababu kila kilichochema kinatoka kwa Baba wa mianga ambaye ni Mungu lakini kwanini wapate kutoka kwenye ufalme mwingine? Sababu kubwa ni kwamba waombaji wengi huwa wanafikiri kupokea majibu ya maombi yao ni simple kumbe sio rahisi kama wanavyofikiri wanaingia kwenye maombi hawana silaha za vita. Mungu ni kweli anawasikia na anawajibu shida inakuja kwenye kupokea majibu ya maombi yao. Kwahiyo falme za giza zikipata nguvu ya kuwashinda malaika wanaokusaidia kupigana vita rohoni kwasababu ya kukosa nguvu. Hizo falme zinaiba majibu ya maombi yao na kuyahifadhi kwenye ufalme wao.Ndio maana mtu akienda kwenye ufalme wao kuomba chochote anapata kumbe ni majibu ya maombi ya watoto wa Mungu yaliibiwa na ufalme wa giza kwa hila. Wengine waliomba wapate watoto, wengine kufanikiwa kwa kila namna na Mungu aliwaahidi kabisa anawapa lakini mpaka leo hii hawajapata! Shida ni nini tatizo ni hila za Shetani na amekushinda kwasababu hukutumia kanuni za kiroho ulipoenda kupigana vita.

          Ni kiu yangu sasa hasira iumbike ndani yako juu ya Shetani ili uweze kupigana vita vya kiroho.Kwasababu kama umeokoka ni haki yako kufanikiwa! Yaani kufanikiwa kwa aliyeokoka ni haki yake. Unachotakiwa kukifanya sasa fuata kanuni za kiroho unapoingia kwenye maombi yako ya vita halafu hata kama Mungu amekuahidi kukupa kitu kwenye maisha yako usiache kuomba. Endelea kusukuma kwa maombi hicho ulichoomba mpaka kitokeee katika macho ya damu na nyama.
           Mungu wabinguni akubariki sana ninaamini kuna eneo umevuka.Mungu akusaidie by
                       Apostle BARAKA SHIBANDA under Godlypowermanifestationministry.

       









Tuesday, November 14, 2017

SOMO: ZIJUE KARAMA KUU TISA ZA ROHO MTAKATIFU ILI ZIWEZE KUKUSAIDIA KATIKA MAISHA YA KIROHO NA KIMWILI.(1WAKORINTHO 12:4-11)

ROHO.
-Ni muonekano wa ndani wa uliobeba uhai wa mtu, bila roho mwanadamu hawezi kuishi/anakuwa amekufa.
Roho imetokana na neno la kilatini linaloitwa "spiritus" lenye maana ya kiingereza breath yaani pumzi! kwahiyo kwa asili roho ya mwanadamu ni pumzi ya uhai!

"Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai" (MWANZO 2:7)
KJV
Then the LORD God formed a the man and dust from the ground and breathed  into his nostrils the breath of life and the man become  a living creature (GENESIS 2:7)
kwahiyo kwa maana nyingine tunaweza kusema huu mstari namna hii
"Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi akampulizia puani (roho) mtu akawa nafsi hai"
Kwahiyo roho ya mwanadamu ina kazi zifuatazo :-
-Kuachilia uhai ndani ya nafsi
-Kuachilia uhai ndani ya mwili ( mavumbi ya ardhi) (YAKOBO 2:26a)
Kwahiyo eneo pekee ambalo Mungu anaweka mahusiano na mwanadamu ni kwenye roho yake mwenyewe!
"Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA, hupeleleza yote yaliyomo ndani yake"(MITHALI 20:27)
KJV
The spirit of man is the lamp of the LORD, searching all inner depth of his heart(PROVERBS 20:27)                                                                                                     Kwahiyo tunaweza kusema " roho ya mwanadamu ni taa ya BWANA, hupeleleza yote yaliyomo ndani yake" Mungu anaachilia mahusiano ndani ya roho ya mwanadamu ili ampe maelekezo yatakayompa nguvu ya kufanikiwa nafsi na mwili.Kwahiyo mafanikio ya mwilini yanategemeana sana na mahusiano uliyonayo na Mungu kwahiyo unatakiwa kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu ili akupe nguvu ya kufanikiwa kimwili.
Mungu ni Roho nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli (YOHANA 4:24), kwahiyo sehemu pekee ambayo Mungu anaweka mahusiano na mtu ni katika roho yake mwenyewe sio katika nafsi au mwili ndio maana Mungu anapomtafuta mtu anatafuta roho yake lengo lake ni kuweka mahusiano na mtu(kuokoka) ili hayo mahusiano yamsaidie kufunguliwa katika vifungo vya nafsi na mwili, Mungu Roho Mtakatifu anatupa nguvu ya kutusaidia sisi kutoka katika vifungo vya nafsi na mwili! Ndio maana maandiko yanasema hivi " Lakini mtapokea nguvuu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu" (MATENDO 1:8a)  kwahiyo tunatakiwa na mahusiano ya karibu sana na Roho Mtakatifu ili tuweze kupata nguvu yait kutuvusha na kututoa katika vifungo vya nafsi na mwili ili tuweze kufanikiwa!

ZIFUATAZO NI NJIA ZA KUFANYA ILI TUWEZE KUWA NA MAHUSIANO  YA KARIBU NA ROHO MTAKATIFU
1.Ongea na Roho Mtakatifu.Roho Mtakatifu ana utu ndani yake kwahiyo unaweza kusema kama vile unavyoweza kusema na mtu mwingine kwasababu Roho Mtakatifu ana maamuzi, nia , matamanio, hisia kwahiyo usiogope kusema na Roho Mtakatifu msemeshe! utaona anavyoanza kuongea nawewe kwasababu Roho Mtakatifu ni Mungu rafiki nia yake ni kutusaidia katika maisha yetu ni Mungu mfariji katika vipindi vigumu vya maisha! kwahiyo ukimchochea kwa namna hii unamruhusu kuingilia kati maisha yako ndio maana maandiko yanasema " usimzimishe Roho" (1 WATHESALONIKE 5:19) kwahiyo ukisema naye atakupa neema ya kuishi maisha yaliyobeba kusudi la Mungu!

2.Mchochee Roho Mtakatifu.Unapomchochea Roho Mtakatifu unamfanya apate kibali cha kuwa karibu nawewe kama andiko linavyosema " usimzimishe Roho" namna hii inatufanya tuwe na mahusiano ya karibu na Roho Mtakatifu, unaweza kumchochea Roho mtakatifu kwa:-
-kufanya maombi ya mfungo
-kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu
-kusoma neno la Mungu

3.Kuwa ni mtu wa rehema.Rehema inaongeza uchaji mbele za Mungu kama jinsi alivyo Roho Mtakatifu yeye ni mtakatifu kwahiyo anafanya kazi pamoja na watakatifu ukitaka Roho Mtakatifu kusema nawe nilazima uwe mtu wa rehema kwa kutumia damu ya Yesu inampa uhalali wa yeye kukaa pamoja nawe na kutenda kazi pamoja nawewe.


NAFSI
-Ni utu halisi wa ndani uliobeba utendaji kazi wa mtu.Nafsi ya mtu imebeba maisha ya mtu bila nafsi huwezi kuwa mtu wa kawaida ili mtu atende kazi sawa sawa na Mungu alivyomuumbia nilazima nafsi yake iwe salama kama sivyo  hawezi kuliishi kusudi la Mungu ! kwasababu kuishi sio kitendo cha kuwa hai ! Kuwa hai  na kuishi ni vitu tofauti ndio maana tunawaona vichaa wako hai lakini hawaishi kusudi la Mungu kwasababu nafsi zao ambazo zimebeba maisha zimefungwa katika ulimwengu wa roho ! kinachofanya nafsi ya mtu yawe ni maisha ni kwasababu imebeba mambo yafuatayo:-
1.Akili
2.Ni
3.Kumbukumbu
4.Fikra
5.Matamanio
6.Utashi
7.Hisia
8.Maamuzi
Ukikosa haya maeneo/ ukifungwa katika ulimwengu wa roho huwezi kuishi maisha yenye kusudi la Mungu !


MOYO.
-Ni kituo kinacho hifadhi taarifa za mtu kwa muda na kuzitoa nje ( kinywani) ambazo kwa asili chanzo chake ni kutoka kwenye nafsi.Kwahiyo moyo wa mtu unatafsiri taarifa zote zilizoko ndani ya nafsi ya mtu ! Kwahiyo ili moyo wako uwe salama lazima ushughulikie nafsi yako vizuri ndio moyo wako utakuwa salama.
"Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni, navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi" (MATHAYO 15:18), kwahiyo ukiona mtu anatamka maneno ya kufeli kwenye maisha yake ujue hilo jambo limetoka moyoni lakini asili yake ni kwenye nafsi yake !


ULIMWENGU WA ROHO
- Ni mahali ambako roho zinaishi, na kuna ulimwengu wa roho katika giza na ulimwengu wa roho katika nuru ambako Roho Mtakatifu ni mwenyeji wetu ndio maana tunapouingia ulimwengu wa Roho tunahitaji msaada wa Roho Mtakatifu ili atupe maelekezo.


ROHO MTAKATIFU
Ni Mungu aliyeziumba mbingu na nchi( MWANZO 1:2b)

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
KARAMA
- N kipawa anachokiachilia Roho Mtakatifu ili kurahishisha utendaji kazj wa mtu kiroho na kimwili.Roho Mtakatifu ndiye aliyebeba karama hizi kwa hakika Roho Mtakatifu yupo ndani ya kila mtu aliyemwamini Yesu Kristo ndani yake ( aliyeokoka) kwahiyo Roho Mtakatifu anazo karama hizi zote ndani ya kila mwamini wa Yesu Kristo lakini kujidhihirisha kwa hizi karama kunategemeana na kiu iliyoko ndani ya mwamini kupokea hizi karama za Roho Mtakatifu.Kwahiyo ukiweka nia ndani yako na kukaa karibu na Roho Mtakatifu utazipokea hizi karama na zitaanza kufanya kazi ndani yako!

1WAKORINTHO 12:4-11Maandiko yanasema hivi " Basi pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule.Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima, na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule, mwingine imani katika Roho yeye yule, na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja, na mwingine matendo ya miujiza, na mwingine unabii, na mwingine kupambanua roho, mwingine aina za lugha, na mwingine tafsiri za lugha, lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye" kutokana na haya maandiko ziko karama saba ambazo Roho Mtakatifu anaziachilia ndani ya mtu kama zifuatazo:-
1.Karama ya neno la hekima
2.Karama ya neno la maarifa
3.Karama ya lmani
4.Karama ya kuponya/uponyaji
5.Karama ya matendo ya miujiza
6.Karama ya unabii
7.Karama ya kupambanua Roho
8.Karama ya aina za lugha/ kunena kwa lugha
9.Karama ya tafsiri za lugha

1:KARAMA YA NENO LA HEKIMA
HEKIMA
- Ni uwezo wa kutumia kitu alichokupa Mungu au kwa maneno mengine ni matumizi sahihi ya uwezo ambao Mungu ameuachilia ndani yako.lnawezekana unajua Mungu lakini je unauwezo wa kutumia maarifa aliyokupa Mungu ili na watu wengine wamjue Mungu uliye naye? Au wewe ni kiongozi wa serikali je una hekima ya kufanya maamuzi katika mambo yote? Wewe ni mfanya biashara je unahekima ya kuendesha biashara yako? Wewe ni mtumishi wa Mungu je una hekima ya kuwashuhudia watu neno la Mungu?

KARAMA YA NENO LA HEKIMA INATUSAIDIA MAMBO YAFUATAYO
1.Inatusaidia kuwa na nguvu ndani yetu."lwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi, Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi.Walakini yafaa kutumia hekima na kufanikiwa"( MUHUBIRI 10:10)." Mtu mwenye hekima ana nguvu, naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo" (MITHALI 24:5).

2.lnatusaidia kuachilia neema katika vinywa vyetu."Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema, bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake" (MUHUBIRI 10:12)

3.Inatusaidia kuwa na mvuto usio na kifani."Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka kwa wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari ya hekima yake"(1WAFALME 4:34)

4.Inatusaidia kuwa na uljnzj ndani yetu." Kwa maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi, na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo"(MUHUBIRI 7:12)

5.Inatusaidia kupigana vita vya kiroho."Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita" (MUHUBIRI 9:18a)

6.lnatusaidia kujipenda/kurunza nafsi zetu."Apataye hekima hujipenda nafsi yake"(MITHALI 19:8)

7.Inatusaidia kuvuta roho za watu kumwelekea Mungu."Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima, na mwenye hekima huvuta roho za watu"(MITHALI 11:30)

Tuangalie kisa cha mfalme Sulemani
Ndipo makahaba wawili, makahaba walimwendea mfalme, wakasimama mbele yake.Na mwanamke mmoja akasema, Ee bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja, nami nilizaa nilipikuwa pamoja naye nyumbani.Kisha, siku ya tatu baada ya kuzaa kwangu, ikawa mwanamke huyu naye akazaa, nasisi tulipokuwa pamoja, hapakuwa na mtu mwingine pamoja nasi nyumbani, isipokusa sisi wawili tu.Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia.Akaondoka kati ya usiku akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa hsingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu.Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu niliyemzaa, kumbe? Amekufa.Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe siyo mtoto wangu niliyemzaa.Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, sivyo hivyo, bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa.Na mwenzake akasema, sivyo hivyo, bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai.Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme.
           Ndipo mfalme akasema, huyu anasema mtoto wangu yu hai, na mtoto wako amekufa.Na huyu akasema sivyo hivyo, bali mtoto wako aliyekufa ni wako, na mtoto aliye hai ni wangu.Mfalme akasema, Nileteeni upanga.Wakaleta upanga mbele ya mfaleme.Mfalme akasema, mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu na huyu nusu.Ndipo mwanamke yule, ambaye mtoto aliye hai ni wake, akamwambia mfalme kwa maana moyoni mwake alimwonea huruma mtoto wake huruma, akasema Ee bwana wangu mpe huyu mtoto aliye hai, wala usimwue kamwe.Lakini yule mwingine akasema asiwe wangu wala wako na akatwe.Ndipo mfalme akajibu akasema , Mpe huyu wa kwanza mtoto aliye hai, maana yeye ndiye mama yake.(1WAFALME 3:16-27)
Hii ni hekima ya ajabu sana ambayo Mungu aliachilia kwa Sulemani haikuwa rahisi kutoa maamuzi magumu ya kuamuru mtoto akatwe hili ni neno la hekima lilimkalia kwenye ndimi zake akatoa maamuzi ambayo hayakuwa kwa ufahamu wake bali Roho Mtakatifu aliachilia neno la hekima ndani yake akafanya maamuzi magumu kibinadamu kakini ndani yake yalikuwa yamebeba majibu ya suala zito lililokuwa mbele yake, nafikiri hata wewe unajiuliza msswali haya kwamba je ingetokea hata mwenye mtoto angesema mtoto akatwe ingekuwaje? Na mfalme Sulemani angechukuliwaje kwenye jamii anayoingoza?  Ingekuwa ni mzozo mkubwa sana lakini kwa kuwa Roho Mtakatifu huyafahamu mawazo ya wanadamu hata bila sisi kuyatambua alimruhusu kuachilia lile neno la hekima kwenye ndimi zake akaamua kwa haki!

Tuangalie kisa kingine cha Yesu Kristo
Hata alipokwisha kuingia hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee na watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakasema, Ni kwa amri gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa amri hii? Yesu akajibu akawaambia, na mimi nitawauliza neno moja, ambalo mkinijibu, ambalo mkinijibu, nami nitawaambia ni kwa amri gani ninatenda mambo haya.Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni au kwa wanadamu? Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, Tukisema, ulitoka mbinguni, atatuambia, mboba basi hamkumwamini? Na tukisema ulitoka kwa wanadamu twaogopa mkutano, maana watu wote wamwona Yohana kuwa ni nabii.Wakamjibu Yesu wakasema hatujui.Naye akawaambia wala mimi siwaambii ninyi ni kwa amri gani ninatenda mambo haya .(MATHAYO 21:23-27)
Haya maswali aliyoukizwa Yesu yalikuwa na mtego mkubwa! Maana walitarajia awajibu majibu mepesi namna hii kwamba ninatenda mambo haya kwa amri yangu na mimi ndiye mwenye hii amri ili wamshitaki kuwa kuwa yeye anajiita Mungu kwahiyo anakufuru! kwa maana hakuna Mungu mwenye mfano wa wanadamu lakini akawauliza maswali ambayo na wao walikosa majibu ya kumpa hilo ni neno la hekima ambalo Roho Mtakatifu aliliachilia kinywani mwake ili awape majibu ambayo atawafunga na mitego waliyokuwa wameitega makuhani na wazee wa watu ili asiingie kwenye mtego waliokuwa wameukusudia! Hii karama ya neno la maarifa anaiachilia Roho Mtakatifu iko mifano mingi kwenye maandiko inayoonyesha ulazima na umuhimu mkubwa wa karama ya neno la hekima inavyoweza kutufanikisha kufanikiwa kwenye maisha yetu ya kila siku kwa nafasi yako soma MATHAYO 22:15-22 wakati mwingine unaweza kudumbukia kwenye mitego kwasababu ya kukosa karama ya neno la hekima "activate your soul now" weka kiu ya kuhitaji hii karama kwa Roho Mtakatifu mwambie rafiki yangu naomba unipe hii karama itende kazi sasa kwenye maisha yako nawe utaona mafanikio makubwa katika huduma yako, uchumi wako maisha yako ya kila siku.

2.KARAMA YA MAARIFA
MAARIFA
-Ni ujuzi ambao Roho Mtakatifu anauachilia ndani ya mtu ambao hakuweza kuujua, ambao unafunua mambo yaliyojificha yenye msaada katika maisha."Kwasababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni" (WAKOLOSAI 1:9)
"Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho.Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu.(1 WAKORINTHO 2:10)
"Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni"(1WAKORINTHO 2:12-13), kwahiyo huu ni ufahamu wa kiroho ambao Roho Mtakatifu anauachilia ili tuweze kuvuka katika maeneo mbali mbali kumbuka bila ufahamu kuna eneo kwenye maisha yako utashindwa kufanikiwa!

FAIDA ZA KUWA NA  KARAMA YA NENO LA MAARIFA
1.Hatuwezi kuangamia kwasababu ya kukosa maarifa."Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa"(HOSEA 4:6a)

2.Hatuwezi kuchukuliwa mateka kwasababu ya kukosa maarifa."Kwasababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa" (ISAYA 5:13a)

3.Inatufanya tuzidi kumjua Mungu."Lakini kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na mwokozi Yesu Kristo"(1YOHANA 3:18), kwahiyo maarifa ya kiroho yanatupa nguvu ya kusogea mbele kutupa hatua nyingine katika maisha.Kwahiyo tunahitaji kuwa na maarifa ya kutisha katika maisha yetu eneo ambalo linatupa maarifa ya kiroho ni kutoka kwenye maandiko(biblia) kwahiyo tunahitaji kuwa na bidii ya kusoma neno la Mungu hata Danieli alipata ufahamu kwa kusoma maandiko kuwa mda wao wa kukaa utumwani umekwisha hakika asibgesoma maandiko asingepata ufahamu wa kujua wanatakiwa watoke utumwani! "Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahausuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli kwa kuvisoma vitabu nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa Yerusalemu, yaani miaka sabini.Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu" (DANIELI 9:1-3) hakika Danieli asingepata ufahamu asingejua anatakiwa afanye nini alipata ufahamu wa kuingia kufanya naombi ya mfungo ili waondoke utumwani! Ni utaratibu mzuri sana wa kuhaikisha unasoma maandiko! (biblia) ( panga utaratibu wa kusoma biblia na kuimaliza ngalau kwa mwaka mara moja)kwasababu majibu ya maombi yetu yapo kwenye maandiko! Pata nafasi ya kusoma vitabu vya watumishi mblimbali ambavyo vinamafunuo ambayo ukisoma unapata vitu ambavyo vinaweza kukufungua ufahamu na ukafanikiwa kwenye eneo ambalo hukukifahamu.
              Roho Mtakatifu ndiye anayeachilia karama ya neno la maarifa inawezekana hufanikiwi kwenye maisha yako kwasababu karama ya neno la maarifa haitendi kazi ndani yako, karama ya maarifa inakupa neema ya kujua hata maeneo uliyofungwa inawezekana unabiashara lakini haufanikiwi! Inawezekana unasoma sana lakini haufanikiwi! Ni mtumishi wa Mungu lakini haufanikiwi  katika huduma yako! Kumbe tatizo sio jitihada zako katika kile ambacho unakufanya kumbe! shida iko kwa uzao wako uliopita ulijiunganisha na miungu ambayo hairuhusu wewe kufanikiwa au hiyo miungu inaweka mipaka ya kufanikiwa kwako kwenye elimu,biashara au utumishi wako usipojua kuwa unatakiwa kujifungua kutoka kwenye hiyo miungu mafanikio yako yatakuwa shida! Roho Mtakatifu ndiye anaachilia hayo maarifa ili ufanikiwe katika maisha yako Muombe Roho Mtakatifu aachilie hii karama ianze kutenda kazi sasa.

3:KARAMA YA IMANI
IMANI
-Ni uhakika wa jambo linalokuja,uhakika ni uhalisia sio jambo la kufikirika kufanyika kwa maana nyingine ni uwezo wa kuishi kile ambacho unauhakika kitatokea kwenye maisha yako, kwa mfano Yusufu aliweza kuishi maono aliyokuwa nayo japo alipitia changamoto nyingi kwenye maisha yake lakini aliamini katika kile kilichokuwa ndani yake mpaka kikatokea (MWANZO 37,38,39,40)
"Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana"(WAEBRANIA 11:1)
KJV
"Now faith is the subsatance of things hoped for, the evidence of things not seen"(HEBREWS 11:1)
Evidence
-ls the fact or reality.
Kwahiyo imani ni uhalisia wa vitu visivyoonekana! Karama ya Roho Mtakatifu inampa mtu uwezo wa kuamua mambo ambayo kwa akili za kibinadamu haikuwezekana! Karama ya lmani ndiyo inayompa mtu nguvu/ uwezo wa kuishi kitu ambacho ana uhakika kitatokea kwenye maisha yako.
       Wakati Eliya alipowakusanya wana wa lsraeli ili ajulikane Mungu anayemwabudu alikuwa na uhakika naye na kusema Mungu atakaye jibu kwa moto na ndiye awe Mungu akajenga madhabahu na kupanga mawe kumi na mbili sawa sawa na kabila kumi na mbili za Israeli akawaambia watu wajaze mapipa manne mara tatu na kuyamwaga kwenye sadaka ya kuteketezwa juu ya kuni akamwita Mungu na moto ukashuka kutoka mbinguni ukateketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni na mawe na mavumbi ukayaramba yale maji yaliyokuwa kwenye ile mifereji.(1WAFALME 18:30-36), imani hii haikuwa yakawaida ni karama ambayo Roho Mtakatifu aliiachilia juu ya Elia ili Mungu aonekane.

Ushuhuda:Yuko mchungaji mmoja ambaye aliwahi kuwa na huduma na wachungaji wenzake kijijini kwahiyo wakaandaa mkutano kuelekea huko kijijini ambako walikuwa walikuwa wanaenda kuwahubiria injili wakaandaa taa za mafuta ya taa wakaelekea kwenye huduma katika hicho kijiji walipofika walifanikiwa kuanza mkutano ulipofika mkutano katikati mafuta ya taa zao yaliwaishia na ilibidi wawe na mafuta ya taa ili waendelee kuhubiri injili wakati wa usiku yalikuwa ni mazingira magumu sana kuhubiri injili bila kuwa na mwanga huyo mchungaji akawaita wachungaji wenzake akasema tuchukue maji tuyageuze yawe mafuta akachota maji kwenye dumu la maji ya lita ishirini akawaambia yeyote anayeamini maji haya yatakuwa mafuta ya taa na aje tufanye maombi wote asiyeamini na asijiunge pamoja nasi tunaoamini wako walioamini na wasioamini salioungana pamoja naye wakaungana kufanya maombi walifanya maombi kwa mda mrefu walipotoka wakachukua yale maji wakajaza kwenye taa zao za mafuta ilikuwa katikati ya mkutano walitumia yale maji yaliyoombewa kuwa mafuta mpaka wakafanikiwa kumaliza mkutano.
        Imani hii aliyokuwa nayo siyo ya kawaida wala sio imani ya kujitahidi ni Roho Mtakatifu ndiye aliyeachilia imani hii ndani yao wakaomba wakiamini Mungu akawafanikisha hakika wangekuwa na hofu wasingefanikiwa kumalizia huk mkutano unajua haikuwa rahisi kwa Shadraki Meshaki na Abedinego kukubali kutupwa kwenye tanuru la moto kwa imani ya kuwa Mungu atawaokoa katika tanuru la moto!(DANIELI 3:16-17), hawakusema ngoja tuu tuabudu sanamu ya mfalme lakini ndani yetu tunamwamini Mungu aliyehai hawakufanya hivyo waliamini kwa Mungu kuwa atawaokoa na Mungu akasimama upande wao! Yako mambo kwenye maisha yako yamekufa unahitaji imani ya kuinua yalikufa yafufuke iwe katika elimu,uchumi huduma uliyonayo unamhitaji Roho Mtakatifu aachilie karama ya imani ndani yako sio kwa namna ya kujitahidi bali ni kwa kuishi uhalisia wa hicho kitu ili kitokee kwenye maisha yako! Muombe Roho Mtakatifu aachilie karama ya imani ianze kutenda kazi sasa.


4:KARAMA YA KUPONYA/UPONYAJI
KUPONYA/UPONYAJI
Ni hali ya kuachilia utendaji wa kawaida wa mtu mkamilifu kiroho/kimwili.Kumfanya mtu ambaye amekuwa mgonjwa kimwili, kiakili au kiroho apate afya njema.
Yaani karama ya uponyaji inashughukikia utendaji kazi wa kawaida wa mwanadamu kama ulivyokuwepo mwanzo kama mtu alikuwa anasikia halafu ikatokea hasikii karama hii ya uponyaji inafanya kazi ya kuponya masikio ya huyo mtu akaanza kusikia tena, kama mtu alikuwa nafsi yake imefungwa kwenye ulimwengu wa roho huyo mtu anafunguliwa na ufahamu wake kwenye maisha unabadilika kufikiri kwake, maamuzi yake, nia yake, utashi wake, akili yake, kumbukumbu yake matamanio na hisia zake zinabadilika.
Kumbuka kuomba ubatizo wa Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu akikubatiza ubatizo huo huwa unaambatana na karama ya uponyaji inayofanya kazi ya kuponya nafsi! kwahiyo hatakama ulikuwa haufahamu umefungwa utaona mabadiliko kwenye maisha yako! Unakuta umebadilika kabisa tofauti na ulivyokuwa mwanzo maana mfumo wa maisha yako unabadilika unaanza kuishi maisha ya rohoni ukiwa duniani kwasababu mambo yaliyokuwa yamefunga nafsi yako yameondoka umekuwa mpya kabisa maana maandiko yanasema ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya! Ni kiu yangu kuona unamuomba Roho Mtakatifu anaachilia karama ya uponyaji ndani yako haiko tuu kwaajili ya kuponya watu tuu miili yao na nafsi zao ipo kwaajili pia ya kuponya nafsi yako ili uweze kufanikiwa kwenye maisha yako.
Unapokuwa umeokoka na unahitaji mafanikio kwenye maisha yako unamhitaji sana Mungu ili akusaidie Roho Mtakatifu aliposhuka kuwa msaidizi wetu (Yohana 14:16) alishuka akiwa kweli ndani yake kajikamilisha na amebeba vitendea kazi ili atufanikishe kwenye maisha yetu muombe Roho Mtatkatifu aachilie hii karama ya uponyaji ianze kutenda kazi sasa.



5:KARAMA YA MATENDO YA MIUJIZA
MIUJIZA
Ni hali ya kuachilia uponyaji ndani ya mtu ambayo kwa hali ya kawaida/kibaolojia isingewezekana.
Karama ya matendo ya miujiza huwa imebeba ndani yake karama ya uponyaji, kwa mfano mtu anaweza akawa alizaliwa akiwa hana mguu karama ya matendo ya miujiza huwa inaachilia uponyaji na kurudisha mguu ambao hakuwa nao au mtu alikuwa amezaliwa akiwa hana macho karama ya matendo ya miujiza huwa inaachilia macho huyo mtu anaanza kuona tena, kanisa la leo tumeipinga hii karama watu wengi hufikiri kila anayetenda miujiza chanzo chake ni cha ibilisi! lakini iko namna ambavyo Mungu anatushangaa wako watu wengi wenye shida mbali mbali wengine hawaoni, wengine hawasikii, wengine hawatembei ni walemavu wamefungwa na ibilisi na haikuwa mpango wa Mungu wawe hivyo ila kwasababu watu ndani yao wameikataa hii karama hawana kiu ya kuipata Roho Mtakatifu ameshindwa kuischilia itende kazi ndani yao maana wengi wamejawa na hofu na kuamini kwamba mtu anayefanya matendo ya miujiza wanatokana na shetani kakini kumbe sivyo! na Yesu akitutazama anatuhurumia maana wako watu ambao alitegemea wafunguliwe lakini anawaona hawajafunguliwa kwasababu watu wamekosa maarifa (HOSEA 4:6) wamekuwa wanyonge hawataki Mungu wao ajitukuze kupitia wao, iko namna Mungu anatamani ajitukuze kupitia hii karama lakini kwasababu watu wengi wameikataa hii karama Mungu anashindwa kujitukuza kupitia sisi.
Kuna wakati wako watu walitamani waone ishara (miujiza) ili wamgeukie Yesu lakini kwasababu hawakuona jambo lolote sameshindwa kugeuza nia zao kama ilivyokuwa kwa Eliya alipoita moto ukashuka toka mbinguni akibadilisha nia za wana wa lsreali waliokuwa na nia mbili hawaelewi Mungu yupi anayestahili kuabudiwa hawajui wamwabudu baali au Mungu aliye hai Eliya alichukuwa maamuzi ndani yake na kumsihi Mungu ajidhihirishe Mungu akashusha moto! watu wote wakasujudu kwamba Mungu anayestahili kuabudiwa ni Mungu wa Eliya (1WAFALME 48:21-39), Roho Mtakatifu anajisikia huzuni kuona Mungu amekosa thamani kwenye maisha ya watu wake kwasababu hawakubali kabisa miujiza na wakati miujiza ipo ili Mungu wetu ahitukuze ni eneo mojawapo ambalo Mungu anaweza kujitukuza Roho Mtakatifu anahitaji watu ambao watakuwa na kiu ya kuona Mungu anajitukuza kupitia hii karama weka kiu ya kuhitaji Roho Mtakatifu aachilie karama ya matendo ya miujiza ili ianze kutenda kazi ndani yako.



6:KARAMA YA UNABII
UNABII
Ni ujumbe ulioongozwa na Roho Mtakatifu, ufunuo kutoka kwa Mungu unaoeleza mambo yanayokuja.
Nabii imetokana na neno prophet
pro- mbele
phemi-kujulisha wazo la Mungu lisilojulikana.

NABII
Ni mtu anayetoa /anajulisha ujumbe uliotoka kwa Mungu usiojulikana.
"Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu na wana wenu na binti zenu watatabiri na vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataota ndoto" (MATENDO 2:17)
Kwahiyo Roho mtakatifu amejifunua kwetu katika kizazi chetu na ameachilia kwa wana na binti kutabiri.

NABII ANA SIFA ZIFUATAZO
1.Ni mtu anayeweza kujua wazo la Mungu la wakati na kulisema/kulitenda.
2.Anapewa neema ya kujua wazo la moyo wa mtu na kulisema
3.Mungu humpa kujua ayaonayo yeye wakati uliopita, uliopo na wakati ujao.

Karama ya unabii huwa inatofauti na nabii karama huwa inatumika pale wakati inahitajika Mungu anapotaka kujulisha watu wake wazo lake linalokuja huwa anaachilia hiyo karama Roho Mtakatifu anawajulisha watu wazo lake wakati ujao kitatokea kitu gani lakini pia hii karama ikikaa ndani ya mtu inamfanya mtu ainuliwe matumaini kwenye maisha yake uko wakati ambao watu walikuwa wamefungwa na ibilisi nafsi zao! na akaweka mioyo yao kuona mbele kushindwa lakini karama hii ikianza kutenda kazi ndani yako unaanza kuona mafaniko yako mbele kwenye maisha yako.

USHUHUDA
Kuna mahali nilipokuwa nasoma tuliwahi kufanya maombi ya kumuomba Mungu atupe majibu kwa wakati huo huo tulipokuwa kwenye maombi tulijawa na ujasiri mwingi na kuamini baada ya maombi hayo Mungu atatupa majibu ya maombi tunayoomba tulipoingia kwenye maombi nilichukuliwa na wingu la kunena kwa lugha ghafla nikaona nawasiliana na Mungu nimeketi naye kwenye kiti kama vile mtu na rafiki yake nikawa namuuliza Mungu maneno haya "Mungu ninataka utupe majibu nikwanini shule fulani (sijapenda kuitaja) hawafiki jointmass? akanijibu akasema nakuambia zaidi ya robo tatu warafika kwenye jointmass hii nikamuuliza tena kwanini na hii shule fulani(sijapenda kuitaja) wameanza kutofika kwenye ibada nikaambiwa sababu ni mkuu wao wa shule amewazuia wasifike lakini jointmass hii watafika watu tisa walikuwa ni viongozi akanitajia na nafasi zao kwenye uongozi na wengine akanitajia majina ndani yangu baada ya kupewa hayo majibu nilijisikia furaha sana nikawa nimemaliza kunena kwa lugha nikawaambia wenzangu tiliokuwa tunaomba nao kwamba jointmass hii shule ambayotulikuwa hatuioni ikihudhuria(sijapenda kuitaja) watafika watu wengi sana nikawaambia pia Mungu kaniambia shule hii (sijapenda kuitaja) watafika watu tisa nikawatajia na baadhi ya majina ya watu ambao nilikuwa nawafahamu miongoni mwao watakatofika, basi tukaendelea kusubiri ni sahihi Mungu alichoniambia siku ya ibada hiyo ya jointmass wakifika ile shule ambayo kwa mda mrefu walikuwa hawahudhurii walikuwa wengi sana baada ya mda nukaendelea kusubiri nione kama kweli ile shule nyingine watakuja watu tisa hakika walikuja watu tisa na wale ambao nililkuwa nimewataja nilimshukuru Mungu kwa kunena kwa lugha.

Iko namna karama ya unabii ikiachiliwa ndani inawapa namna ya kuona vitu vilivyoko mbele ambavyohamkuweza kuvijua.

FAIDA ZA KARAMA YA UNABII
1.Inatusaidia kujua mitego ya shetani iliyoko mbele yetu
2.Inatusaidia kujua ukweli uliofichika katika ulimwengu wa roho.



7:KARAMA YA KUPAMBANUA ROHO
KUPAMBANUA
-Maana yake ni kuchanganua/kufichua.
KUPAMBANUA ROHO
-Ni karama inayotofautisha roho zinazotenda kazi huku zikijifananisha na Roho wa Mungu na wakati sio.
      "Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu kwasababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani"(1YOHANA 4:1)

FAIDA YA KARAMA YA KUPAMBANUA ROHO
1.Inatusaidia kututenga na kila roho zinazotaka kufanya uteka.
2.Inatusaidia kujua roho zingeweza kuleta madhara katika ulimwengu wa roho.



8:KARAMA YA AINA ZA LUGHA/KUNENA KWA LUGHA
KUNENA KWA LUGHA
- Ni kuongea kwa lugha.

AINA ZA KUNENA KWA LUGHA
1.Kunena kwa lugha za mbinguni(malaika)/mpya.
MARKO 16:16

2.Kunena kwa lugha za wanadamu
MATENDO 2:1-11

FAIDA ZA KUNENA KWA LUGHA
1.Hutujenga nafsi zetu.
1WAKORINTHO 14:4

2.Hutusaidia kuomba maombi yetu mbele za Mungu kwa siri.
1WAKORINTHO 14:2

3.Inatusaidia kuomba kwa mda mrefu




9:KARAMA YA KUFASIRI LUGHA/KUTAFSIRI LUGHA
1WAKORINTHO 14:13
Lengo la karama ya kufasiri lugha ni ili kanisa liweze kujengwa.lnategemea karama ya kunena kwa lugha

Karama hii ya kutafsiri lugha inategemeana na mazingira ya unenaji wa hiyo lugha
1.Mtu akiwa anazungumza na mtu kwa njia ya maombi.
2.Mtu akiwa anazungumza na watu wake kwa njia ya lugha
Roho Mtakatifu anaweza kuachilia msuko wa kufasiri kwa mtu aliyebeba karama ya kutafsiri lugha.






Sunday, November 12, 2017

 SOMO:FAHAMU THAMANI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA YAKO.
UFAHAMU.
-Ni uelewa juu ya/kuhusu kitu fulani.
THAMANI.
-Ni heshima inayostahili kumpa mtu/kitu fulani.
ROHO MTAKATIFU
-Ni Mungu aliyeziumba mbingu na nchi. Roho ikatulia juu ya uso wa maji (Mwanzo 1:2b)
MAISHA
-Maisha ni nini?
Maisha ni hali ya kuwa na utendaji kazi kamilifu sawa sawa na Mungu alivyomuumbia mwanadamu.Maisha sio kitendo cha kuwa hai ni hali ya kuwa na utendaji kazi kamilifu sawa sawa na Mungu alivyomuumbia mwanadamu alipokuwa katika bustani ya Eden.
Maisha ambayo Mungu alimuumbia mwanadamu ilikuwa ni nafsi ya mtu kwasababu Mungu alimzawadia mwanadamu maisha ili aishi vile alivyokuwa anataka kuishi wakati wote atakapokuwa bustani ya Edeni ambayo hayo maisha ni nafsi! bila nafsi haiwezekani kuishi maisha! uwe na uhakika nafsi yako ikifungwa katika ulimwengu wa roho huwezi kuishi maisha halisi ambayo Mungu alikukusudia kuishi utakapokuwa duniani.

Kwanini nafsi ya mtu ni maisha?
Asili ya maisha ya mtu yameanzia katika ulimwengu wa roho Mungu alipomuumba mwanadamu alihakikisha anaweka mahitaji yote ambayo mwanadamu anayahitaji halafu akayakusanya na kuyaweka pamoja kwenye nafsi alivyomuumbia mwanadamu, Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai(Mwanzo 2:7)

Nafsi ni nini?
Nafsi ni utu wa ndani/ ni mtu halisi wa ndani, huu utu halisi wa ndani ndio uliobeba utendaji kazi kamilifu wa mwanadamu.
Nafsi ya mtu imeumbwa na mambo yafuatayo:-
1.Akili
2.Nia
3.Utashi
4.Maamuzi
5.Hisia
6.Matamanio
7.Fikra
8.Kumbukumbu
Bila kuwa na nafsi hakuna maisha ukifungwa kwenye ulimwengu wa roho nafsi yako hata eneo moja kati ya vitu vilivyoumbwa ndani ya nafsi yako huwezi kuishi maisha halisi aliyoyakusudia Mungu kwenye maisha yako, shetani kazi yake ni kuharibu maisha yako lakini Yesu alikuja ili wanadamu wawe na uzima(maisha) Yohana Mtakatifu 10:10(soma english translation) baada ya mwanadamu kufanya dhambi! chanzo chake ni katika bustani ya Edeni.Tangu mwanadamu kutenda dhambi amekuwa akiishi maisha kinyume na mpango wa Mungu lakini Mungu alimtuma Yesu ili kuachilia maisha tena kwa mwanadamu ili aishi ndani ya kusudi la Mungu.Yesu alipoondoka duniani alimwacha Roho Mtakatifu ili aendeleze maisha ya mwanadamu.Roho ndiyo itiayo uzima mwili haufai kitu maneno hayo niliyowaambia ni roho tena ni uzima (Yohana 6:63)(soma english translation)

Kwanini tunatakiwa kumpa thamani Roho Mtakatifu?
1.Roho Mtakatifu Mungu anayejidhihirisha katika majira tuliyonayo(Yohana 14:16-17)
2.Roho Mtakatifu anaukamilifu ndani yake(Wagalatia 4:1-7)
3.Roho Mtakatifu ni msaidizi aliyebeba vitendea kazi vinavyotusaidia katika maisha (1Wakorintho 12:4-11)
4.Roho Mtakatifu ni wakili msimamizi wa urithi wa ahadi zote alizotupigania Yesu msalabani(Waefeso 1:13-14)
5.Roho Mtakatifu ndiye anayetupa maisha (YOHANA 6:63)