Sunday, November 12, 2017

 SOMO:FAHAMU THAMANI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA YAKO.
UFAHAMU.
-Ni uelewa juu ya/kuhusu kitu fulani.
THAMANI.
-Ni heshima inayostahili kumpa mtu/kitu fulani.
ROHO MTAKATIFU
-Ni Mungu aliyeziumba mbingu na nchi. Roho ikatulia juu ya uso wa maji (Mwanzo 1:2b)
MAISHA
-Maisha ni nini?
Maisha ni hali ya kuwa na utendaji kazi kamilifu sawa sawa na Mungu alivyomuumbia mwanadamu.Maisha sio kitendo cha kuwa hai ni hali ya kuwa na utendaji kazi kamilifu sawa sawa na Mungu alivyomuumbia mwanadamu alipokuwa katika bustani ya Eden.
Maisha ambayo Mungu alimuumbia mwanadamu ilikuwa ni nafsi ya mtu kwasababu Mungu alimzawadia mwanadamu maisha ili aishi vile alivyokuwa anataka kuishi wakati wote atakapokuwa bustani ya Edeni ambayo hayo maisha ni nafsi! bila nafsi haiwezekani kuishi maisha! uwe na uhakika nafsi yako ikifungwa katika ulimwengu wa roho huwezi kuishi maisha halisi ambayo Mungu alikukusudia kuishi utakapokuwa duniani.

Kwanini nafsi ya mtu ni maisha?
Asili ya maisha ya mtu yameanzia katika ulimwengu wa roho Mungu alipomuumba mwanadamu alihakikisha anaweka mahitaji yote ambayo mwanadamu anayahitaji halafu akayakusanya na kuyaweka pamoja kwenye nafsi alivyomuumbia mwanadamu, Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai(Mwanzo 2:7)

Nafsi ni nini?
Nafsi ni utu wa ndani/ ni mtu halisi wa ndani, huu utu halisi wa ndani ndio uliobeba utendaji kazi kamilifu wa mwanadamu.
Nafsi ya mtu imeumbwa na mambo yafuatayo:-
1.Akili
2.Nia
3.Utashi
4.Maamuzi
5.Hisia
6.Matamanio
7.Fikra
8.Kumbukumbu
Bila kuwa na nafsi hakuna maisha ukifungwa kwenye ulimwengu wa roho nafsi yako hata eneo moja kati ya vitu vilivyoumbwa ndani ya nafsi yako huwezi kuishi maisha halisi aliyoyakusudia Mungu kwenye maisha yako, shetani kazi yake ni kuharibu maisha yako lakini Yesu alikuja ili wanadamu wawe na uzima(maisha) Yohana Mtakatifu 10:10(soma english translation) baada ya mwanadamu kufanya dhambi! chanzo chake ni katika bustani ya Edeni.Tangu mwanadamu kutenda dhambi amekuwa akiishi maisha kinyume na mpango wa Mungu lakini Mungu alimtuma Yesu ili kuachilia maisha tena kwa mwanadamu ili aishi ndani ya kusudi la Mungu.Yesu alipoondoka duniani alimwacha Roho Mtakatifu ili aendeleze maisha ya mwanadamu.Roho ndiyo itiayo uzima mwili haufai kitu maneno hayo niliyowaambia ni roho tena ni uzima (Yohana 6:63)(soma english translation)

Kwanini tunatakiwa kumpa thamani Roho Mtakatifu?
1.Roho Mtakatifu Mungu anayejidhihirisha katika majira tuliyonayo(Yohana 14:16-17)
2.Roho Mtakatifu anaukamilifu ndani yake(Wagalatia 4:1-7)
3.Roho Mtakatifu ni msaidizi aliyebeba vitendea kazi vinavyotusaidia katika maisha (1Wakorintho 12:4-11)
4.Roho Mtakatifu ni wakili msimamizi wa urithi wa ahadi zote alizotupigania Yesu msalabani(Waefeso 1:13-14)
5.Roho Mtakatifu ndiye anayetupa maisha (YOHANA 6:63)







No comments:

Post a Comment